Breaking

Friday 4 March 2022

WANAFUNZI WA TANZANIA WARUHUSIWA KUPITA MPAKA WA URUSI




Wanafunzi wa Kitanzania walio katika mji wa Sumy nchini Ukraine wameruhusiwa kutoka nchini humo kupitia mpaka wa Russia baada ya mazungumzo ya kidiplomasia kufanyika na Serikali ya Russia kuridhia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo ijumaa Machi 04, 2022 na Balozi za Tanzania nchini Sweden pamoja na  Urusi imeeleza kuwa shughuli ya kuwatoa wanafunzi wote kutoka Sumy hadi kwenye mpaka wa Russia, litaratibiwa na Serikali hiyo na tayari imeanza mipango ya utekelezaji.

“Wanafunzi hao watakapofika mpakani, Ubalozi wa Tanzania nchini Russia utawapokea kwa taratibu nyingine za kurejea nyumbani,” inaeleza taarifa hiyo ya Balozi hizo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa kwamba wakati shughuli ya kuwatoa wanafunzi walioko Sumy ikiendelea kuratibiwa, Balozi zinaomba wanafunzi hao pamoja na wazazi kuwa wavumilivu ili kuhakikisha wanatoka kwa usalama nchini Ukraine.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages